Beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein Tshabalala, amesikia kwamba Yanga wanaitaka saini yake kwa udi na uvumba na alichowaambia ni kwamba wasahau mpango huo.
Tshabalala ni miongoni mwa nyota walionasa katika
Rada za kocha Hans Van Pluijm kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake msimu ujao
wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
Tashabalala amesema kuwa hafikirii kuitema Simba na
kutimkia Yanga kwani ndoto zake kubaki Msimbazi ili kuifanyia makubwa msimu
ujao wa Ligi Kuu
“Nimesikia kwamba Yanga wanaitaka saini yangu ingawa bado sijafuatwa na kiongozi yeyote, lakini hata kama ikiwa ni kweli watanifuata sina mpango wa kuondoka Simba kwani bado nina mkataba wa mwaka mmoja Simba”, alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni