Wakati zoezi la umwagiliaji wa dawa za kuua mbu maarufu kama dawa za ukoko likiendelea mkoani Geita zoezi hilo limekubwa na changamoto kubwa kutokana na wananchi kushindwa kutoa ushirikiano kwa wamwagiliaji wakidai kuwa dawa hizo zinasababisha ongezeko la wadudu kama kunguni katika nyumba zao pamoja na kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wananume.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanyunyuziaji wa dawa hizo mkoani hapa walipokuwa wakizungumza na Storm habari mapema hii leo ambapo wamesema kuwa wananchi wamekuwa wakishindwa kutoa ushirikiano kutokana na kuamini kuwa dawa hizo zinasababisha upungufu wa nguvu za kiume na ikiwemo kuongezea kwa wadudu hali ambayo inasabishwa zoezi hiloo kushindwa kufanyika ipasavyo.
Hata hivyo storm habari imezungumza na mratibu mthibiti wa malaria kutoka katika halimashauri ya mji wa Geita bi Rachel Masuke ambapo amesema kuwa suala hilo halina ukweli wowote ndani yake kwani dawa hizo zimetolewa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoeneza magonjwa ikiwemo mbu pamoja na wadudu wengine.
Aidha Rachel amewataka wananchi kuachana na imani hzo kwa kukubali nyumba zao zinyunyuziwe kwani lengo la serikali ni kuhahaikisha inapunguza kasi ya maambukizi ya maralia nchini na sio kuongeza wadudu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni