WANANCH MKOANI GEITA WAMETAKIWA KUHAKIKISHA
WANAIMARISHA ULINZI KATIKA MITA ZAO ZA
MAJI AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIFUNGWA KATIKA NYUMBA ZAO KWA KUZIJENGEA UZIO ILI
KUEPUSHA WIZI AMBAO UMEIBUKA KATIKA MAENEO MENGI MKOANI HAPA.
KAULI HIYO IMETOLEWA LEO NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA
MAMLAKA YA MAJI SAFI NA TAKA MKOANI HAPA(GEUWASA) BW ISACK MGENI, ALIPOKUWA
AKIZUNGUMZA NA TAA YA JAMII OFISINI KWAKE BAADA YA WANANCHI WA MTAA WA KATOMA
KULALAMIKIA KUKITHIRI KWA WIZI WA MITA JAMBO AMBALO LIMELETA CHANGAMOTO KUBWA
KWA WAKAZI WA ENEO HILO IKIWEMO ONGEZEKO LA GHARAMA ZA MALIPO.
HATA HIVYO KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI AMETOA UFAFANUZI JUU YA
MASWALI YALIYOKUWA YAKIULIZWA NA WANANCHI MBALIMBLI KUTAKA KUJUA NINI SABABU ZA
MITA HIZO KUFUNGWA NJE YA NYUMBA ZAO AMBAPO AMESEMA KUWA WANALAZIMIKA KUFANYA
HIVYO ILI KURAHISISHA USOMAJI WA MITA KUTOKANA NA WANANCHI WENGI KUWA NA NYUMBA
ZILIZOKO NDANI YA UZIO.
AWALI WANANCHI WA MTAA WA KATOMA MKOANI HAPA WALIILAMIKIA
MAMLAKA HIYO KWA KUFUNGA MITA ZA MAJI NJE YA UZIO WA NYUMBA ZAO HALI AMBAYO
IMEKUWA NI CHANGAMOTO KWAO KUTOKANA NA MITA HIZO KUIBIWA JAMBO AMBALO
LINASABABISHA KUONGEZEKA KWA GHARAMA ZA MALIPO PINDI WAENDAPO KULIPIA.
mamlaka ya maji ingebuni na kuelekeza umma namna bora ya kuzijengea hizo mita za maji ili msomaji aweze kusoma mita bila kuingia ndani ya geti au nyumba ya mteja na mwizi pia asiweze kuziiba.
JibuFuta