WAFANYABIASHARA WOTE NCHINI WAMETAKIWA KUACHA TABIA YA KUBADILISHAJI
MIFUMO YA SIMU BANDIA (KUFLASHI) ILI KUWAHADA WANANUNUZI WAO.
KAULI HIYO IMETOLEWA LEO NA MENEJA WA MAMLAKA YA MAWASILIANO
TANZANIA (TCRA) INNOCENT MUNGI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA KAIMU
MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAWASILIANO NCHINI KATIKA SEMINA NA WADAU MBALIMBALI
WA MAWASILIANO JUU YA UFAHAMU WA MFUMO WA
RAJISI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO WA SIMU ZA MKONONI (CEIR) ILIYOFANYIKA KATIKA
UKUMBI WA OFISI ZA MKUU WA MKOA WA GEITA.
AMESEMA KUWA LENGO LA MFUMO HUO WA UTAMBULISHO WA SIMU ZA
VIGANJANI UNALENGO LA KUONGEZA USALAMA MTANDAONI KWA WATUMIAJI WA SIMU KUZUIA MATUMIZI
YA SIMU ZISIZO NA KIWANGO PAMOJA NA KUTHIBITI WIZI WA SIMU HUKU AKIDAI KUWA
YEYOTE ATAKAYEKIUKA AGIZO HILO HATUA KALI ZA KISHERA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
AIDHA KWA UPANDE WAKE MKUU WA MKOA WA GEITA AMBAYE ALIKUWA
MGENI RASMI KATIKA SEMINA HIYO YA WADAU WA MAWASILIANO MH.EZEKIEL KYUNGA AMEWAPONGEZA
WAWEKEZAJI WALIOCHANGIA UKUAJI WA SEKTA YA MAWASILIANO NCHINI KWANI UJIO WAO
UMECHANGIA KUPUNGUA KWA GHARAMA ZA SIMU IKIWA NI PAMOJA NA KUONGEZA PATO LA
TAIFA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni