Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi
Taarifa ya jeshi la polisi imeeleza kuwa mnamo tarehe 27.06.2016 majira ya saa 12:00 jioni katika kitongoji cha Moha kijiji cha Ilungu kata ya Nyigogo tarafa ya Itumbili wilaya ya Magu mkoani Mwanza, mtoto aliyejulikana kwa jina la Julius Leonard miaka [7] mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi ilunga aliuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake wa kambo aitwaye Leonard Joseph miaka [32] mkulima na mkazi wa kijiji cha Ilunga.
Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi wa awali na daktari na kuonekana ukiwa na alama za fimbo huku mguu wa kushoto ukionekana kuvuja damu kwa ndani kutokana na adhabu ya fimbo hizo.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ametoroka baada ya kuona amefanya mauaji.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana natukio hilo, huku msako wa kumsaka na kumtia nguvuni mtuhumiwa wa mauaji tajwa hapo juu ukiwa unaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi akiwataka kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi, kwa kutoa taarifa za mtuhumiwa wa mauaji haya mahali alipo ili awezwe kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za aina kama hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni