Serengeti Boys wameibuka na ushindi wa
mabao 3-0 dhidi ya Malaysia katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu katika
michuano ya vijana ya AIFF ya nchini India.
Ushindi huo unaipa Serengeti Boys nafasi ya tatu kupitia mabao matatu yaliyofungwa na Rashid Abdallah katika dakika ya 13, Shabani Zubeiri katika dakika ya 41 na Mushin Malima akamalizia bao la tatu katika dakika za lala salama za kipindi cha kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni