Mo ‘awachana’ viongozi Simba - KONA YANGU

ELIMU MICHEZO NA BURUDANI

https://msashavideos.blogspot.com/

Post Top Ad

Responsive Ads Here
Mo ‘awachana’ viongozi Simba

Mo ‘awachana’ viongozi Simba

Share This

MFADHILI wa zamani na mwanachama wa Klabu ya Simba, bilionea Mohammed Dewji `Mo’ ameungana na wanachama wengine wa klabu hiyo kuelezea kuchoshwa na kuvurunda kwa timu yao katika michuano ya Ligi Kuu ya soka nchini.

Simba juzi ilimalizia msimu kwa kulazwa 2-1 na JKT, kikiwa kipigo cha sita msimu huu, viwili kutoka kwa watani wao Yanga waliotwaa ubingwa kwa msimu wa pili hivi karibuni, huku Simba kwa msimu wa nne mfululizo ikiishia kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, na hivyo kushindwa kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.
Kutokana na hali hiyo, Dewji aliibuka na kutoa ya moyoni kupitia mtandao wake wa twitter, akisema; “Simba mnatunyima raha, tumechoka kutaniwa na kutukanwa mitaani.” Kwa kauli hiyo, ameonesha kuungana na idadi kubwa na Wanasimba wasioridhishwa na maendeleo ya klabu hiyo ambayo kwa mara ya mwisho ilitwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2011/2012.
Wanasimba hao ambao juzi na jana wamemuunga mkono Mo, kwa nyakati tofauti wamekuwa wakishinikiza uongozi uwajibike kwa kushindwa kuipa timu mafanikio, huku mahasimu wao Yanga wakichanua katika ligi kushiriki katika michuano ya kimataifa kila mwaka.
Mwaka huu, Yanga imefika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ilikoangukia baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa na Al Ahly ya Misri, hivyo kuzidisha `mikogo’ dhidi ya wenzao wa Simba.
Mo anakumbukwa kwa mafanikio makubwa aliyoipa Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000, ikiwa ni pamoja na kuivusha kwa kishindo hadi hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwavua ubingwa walikuwa watetezi, Zamalek ya Misri. Kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Ltd - (MeTL) ambayo Mo ni Rais na Mkurugenzi Mtendaji wake, ndiyo iliyokuwa inaifadhili Simba.
Na mwishoni mwa mwaka jana, Mo aliibuka na kutangaza kuwa tayari kuinunua klabu hiyo kwa dau la Sh bilioni 20 ili aiendeshe kisasa zaidi iweze kwenda sambamba na kasi ya klabu kubwa mithili ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Hata hivyo, uongozi wa Simba chini ya Rais wake, Evans Aveva ulikataa kwa visingizio kadhaa, ikiwa ni pamoja na kumtaka apandishe dau ikielezwa thamani ya Simba ni zaidi cha kiwango hicho cha fedha.
Pamoja na maelezo hayo, Mo aliwataka kutafakari uamuzi wao, akisisitiza dhamira yake ni njema kwa Simba, kwani pamoja na mambo mengine, inayumba na kukosa mwelekeo kutokana na kutokuwa na fedha za kuifanya ijiendeshe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages