MAMA JANET MAGUFULI AWATAKA WATU KUENDELEA KUSAIDIA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI - KONA YANGU

ELIMU MICHEZO NA BURUDANI

https://msashavideos.blogspot.com/

Post Top Ad

Responsive Ads Here
MAMA JANET MAGUFULI AWATAKA WATU KUENDELEA KUSAIDIA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

MAMA JANET MAGUFULI AWATAKA WATU KUENDELEA KUSAIDIA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

Share This















Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi walipomtembelea leo asubuhi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kujikinga na mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa wakifurahia jambo na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kujikinga na mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi..



Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kuzia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo aliiasa jamii kujali kundi hili na kuacha imani potofu dhidi yao. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said mafuta ya kuzuia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi leo Ikulu ndogo ya Mkoa wa Lindi.Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa














Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akikabidhi zawadi ya mbuzi na kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa



Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi wakiwa katika picha ya Pamoja na jamii ya watu wenye ulemavu leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages